MUIGIZAJI YUSUPH MLELA AJITOSA RASMI KWENYE UBONDIA
Taarifa nyingine kutoka kiwanda cha Bongomovie ni hii inayomuhusu Yusuph Mlela ambaye ametangaza rasmi kuingia kwenye ubondia na yuko tayari kwa pambano muda wowote.
“Nimeingia kwenye ubondia lakini sio kama nimeacha kucheza filamu. Kwa sasa filamu zangu nafanya nchini Kenya na zinaonyeshwa kwenye kituo kikubwa hapa nchini Tanzania. Nimeingia kwenye ubondia kwa sababu hiki ni kitu ambacho nilikuwa nakipenda tangu utotoni.” Alisema Yusuph Mlela.
Aidha msanii huyo wa filamu aliongeza kuwa yupo kwenye maandalizi ya pambano kati yake na Nay wa Mitego na kwamba haogopi kupambana na mtu yeyote ilimradi tu awe kwenye uzito sawa na wake. “Kuna promoter alinifata kwa ajili ya kuaadaa
pambano mimi na Nay wa Mitego lakini bado tupo kwenye maongezi. Simuogopi mtu yeyote ili mradi awe kwenye uzito wangu nitakuwa niko tayari kupigana naye.”