Breaking News

JOHN HECHE AFUNGUKA KUHUSU RIPOTI YA MADINI...HAYA HAPA MAAMUZI YAKE



Mbunge John Heche amesema wananchi hawataruhusu ndege kutua North Mara kuchukua madini kwa sababu kampuni hiyo imebainika kuiibia nchi.

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amesema atawahamasisha wananchi kuvamia mgodi wa North Mara baada ya ripoti kuonyesha unaiibia nchi.

Mbunge Heche amemtaka Rais kupeleka mabadiliko ya Katiba bungeni ili kuruhusu marais Mkapa na Kikwete wachunguzwe kuhusiana na mikataba ya madini.