Breaking News

BAADA YA RIPOTI YA PILI KUWASILISHWA....MBATIA ADAIBUNGE LINAHUSIKA KWA MIKATABA MIBOVU YA MADINI




Mbunge wa Vunjo Mb James Mbatia amesema Bunge ndilo la kulaumiwa hasa wabunge wa CCM kwa kupitisha mikataba mibovu kwa ushabiki bila kupambanua na kudadavua mikataba hiyo kwa maslahi ya Taifa. 

Aidha amedai kuwa mwaka 1998 wakati mikataba hiyo ya madini ikiletwa bungeni ilipitishwa tu bila kuwa na uelewa na elimu kuhusu biashara ya madini duniani.

Hayo yameibuka baada ya Rais Magufuli kuunda tume mbili tofauti za kuchunguza mchanga wa madini uliokuwa ukisafirishwa kwenda nje ya nchi kinyemela.