WHITEDENT YAONGOZA TUZO YA SUPER BRAND 2017...ITV,MWANANCHI,PEPSI,FOMA GOLD NAO PIA HAWAJASAHAULIKA

Akiongea kuhusu matokeo ya chapa bora zinazokubalika wa kiasi kikubwa
nchini, Afisa Mtendaji wa taasisi ya The Centre for Brand
Analysis,Stephen Cheliotis,alisema kuwa inafurahisha kuona chapa nyingi
za Tanzania zinaendelea kushikilia rekodi ya ubora na kuendelea kupata
tuzo SuperBrand mwaka hadi mwaka wakati huohuo zikijitokeza chapa mpya
ambazo zinafanya vizuri kwenye masoko.
‘’Mwaka huu chapa nyingi zimeweza kuendelea kushikiria rekodi ya kuingia
kwenye chapa bora 20 zinazoongozwa kwenye masoko na mwaka huu chapa za
bidhaa kwenye kundi la usafi na afya za Whitedent na Foma Gold zimefanya
vizuri na katika utafiti wetu tumegundua kuwa zinakubaliwa na wengi
kwenye masoko kutokana na kuwa na viwango vya juu vya ubora" alisema
Stephen Cheliotis.
Amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam
wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ukihusisha pia
makampuni ya hapa hapa nchini yanayotumia nembo cha chapa za biashara za
kimataifa kama vile TOYOTA na Pepsi ambapo chapa 10 zimeendelea kuingia
kwenye chapa 20 bora na utafiti huo ulifanyika katika mgawanyo wa
makundi ya taasisi za fedha,vyakula na vinywaji, magari na utoaji wa
huduma kwa jamii.