Breaking News

WANANCHI WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AMPANDISHE CHEO ASKARI ALIYEFYATUA RISASI JANA MBELE YA ADAM MALIMA.


Image result for jamii forumKufuatia tukio lililotokea jana Jumatatu kuhusu askari kufyatua risasi mbele ya Adam Malima,kitendo hicho kimejadiliwa kwa namna tofauti miongoni mwa wananchi walioshuhudia tukio hilo.

Wapo walio chukizwa na kitendo hicho wakidai kwamba askari hakutakiwa kufanya vile mbele ya waziri huyo wa zamani mhe. Adam Kighoma Malima.Lakini mdau mmoja kupitia mtandao wa Jamiiforums yeye ameonesha kufurahishwa na hali hiyo akidai kwamba watanzania wote wako chini ya sheria kwahiyo ni muhimu "Utii wa sheria bila shuruti".Mwananchi huyo amemshauri Rais John Pombe Magufuli kumpandisha cheo askari polisi huyo aliyefyatua risasi tatu hewani na kufanikisha kumkamata na kumfikisha kituoni mtuhumiwa Adam Malima.Maoni yake ni haya;

"Wewe ukiwa kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,sisi Watanzania wenye nia njema na Nchi hii tunaomba umfikirie askari yule aliyekumbana na kadhia ya maneno ya kejeli toadam kwa Adam Malima na kikundi chake,walau mpe hata "V" moja kwa ushupavu wake.

Askari wetu wamekuwa wakitulinda usiku na mchana lakini bado hatujawahi kutambua thamani yao,tumekuwa watu wa "kuwadhihaki" tu.

Maneno ya dharau na kejeli kama yale hayavumuliki kwa mtu wa kawaida,sembuse kwa askari ambaye yupo katika majukumu yake. JPM mpandishe cheo askari yule kwa uvumilivu wake uliotukuka,vinginevyo mida hii kuna watu wangekuwa mochwari kwenye mafriji.

Ujumbe wangu natumai umefika" alimalizia mwananchi huyo huku akiwa na imani kuwa ujumbe wake umefika.