SHILOLE AFUNGUKA ISHU YAKE YA KUFANYA KOLABO NA NICK MINAJ...ADAI JLo ALILETA MIZINGUO FLANI HIVI.

Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ametoa ufafanuzi wa kushindikana
kufanya kolabo yake na Jennifer Lopez(JLo) ambayo msanii huyo alitangaza
kufanya nae.
Shilole amesema kuwa alisha onana na meneja wa msanii huyo kutokea
Marekani na kuongea nae kuhusu mpango wake wa kufanya kolabao, lakini
baadae ilishindikana hivyo naye ameshindwa kwenda tena Marekani kutokana
na kuwa busy.
“Nilishindwa kurudi tena Marekani kutokana na mambo niliokuwa nayo
ikiwemo ya kifamilia na pia Jlo nae alikwa busy busy na nyimbo yake ya
“Ain’t your mama” nikaona basi tusisumbuane sana mwache aendelee na
mambo yake, ila nitamfuta Nick Minaj.


