RAIS MAGUFULI AKABIDHI UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KWA RAIS MUSEVENI WA UGANDA
Rais John Magufuli jana (Jumamosi) amekabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais Yoweri Museveni.
Muda
mfupi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo, Rais Magufuli ambaye alikuwa
mwenyekiti wa EAC kwa miaka miwili amewashukuru wanachama wa jumuiya
hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo miezi michache baada ya kuingia
madarakani.
“Mliniamini
mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema Rais
Magufuli ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa EAC, mapema mwaka jana.
Rais Magufuli amesema anaimani na Rais Museveni kuwa atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake.
“Yaliyonishinda kuyatatua, atayatatua yeye (Rais Museveni),”amesema.
Mara
baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Museveni ambaye sasa ni
mwenyekiti wa EAC amesema atahakikisha anatumikia nafasi hiyo kwa nguvu
na uwezo wake wote.