MAREKANI NA SAUDI ARABIA ZASAINI MIKATABA KUKABILIANA NA VITISHO VYA IRAN
Makubaliano
ya ununuzi wa silaha za thamani ya dola za Kimarekani bilioni 110
ambayo yamesainiwa na Marekani na Saudi Arabia Jumamosi yanakusudia
kutokomeza uchochezi hatarishi wa Iran.
Hayo
yamesemwa Jumamosi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson
wakati wa mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia.
Akizungumza
katika mkutano wa pamoja Riyadh na Waziri wa Mambo ya Nje Adel
al-Jubeir, Tillerson amesema mkataba huo wa ulinzi umekusudia kusaidia
“mkakati wa ulinzi wa muda mrefu wa Saudi Arabia na eneo lote la Ghuba
ya Uajemi.”
Mkataba
huo tayari umekwisha pitishwa, Tillerson amesema, “katika hali ya hivi
sasa ya kupambana na kampeni hatarishi ya Iran na vitisho vyake, ambavyo
vipo katika maeneo yote ya mipaka ya Saudi Arabia.”
Mkataba
huo wa ulinzi ambao unaanza mara moja, ni moja kati ya mtiririko wa
mikataba iliyosainiwa Jumamosi na Mfalme wa Saudi Arabia Salman na Rais
Donald Trump.
Imelenga
katika kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kibiashara kati ya nchi
hizo mbili na unajumuisha mkataba wa pili wa ulinzi ambao unahiari
mbalimbali zenye thamani ya mpaka dola billioni 350 kwa kipindi cha
miaka 10 ijayo.
Tillerson
amesema lengo la Trump kufanya ziara Saudi Arabia ilikuwa kukabiliana
na aina yoyote ya vitisho vinavyofanywa na Iran. Amesema mlolongo wa
mikutano ya hadhara na ya ndani ambayo Trump amekuwa akiifanya inalengo
la “kupeleka ujumbe mzito kwa maadui zetu wanaofanana.”
Tillerson
amemtaka rais aliyechaguliwa tena Iran Hassan Rouhani kutumia kipindi
chake cha pili madarakani kusitisha programu ya kombora la balistiki
nchini humo na tabia ya nchi yake kusaidia magaidi.