Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya
SportPesa Pavel Slavkov akikabidhiana hati ya makubaliano ya mkataba na
Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva ukiwa ni mkataba wa udhamini wa
kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo
katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya
SportPesa Pavel Slavkov pamoja na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva
wakisaini hati ya makubaliano ya mkataba na ukiwa ni mkataba wa udhamini
wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo
katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa SportPesa
Tanzania Abbas Tarimba.
Kampuni ya SportPesa imeingia mkataba wa miaka mitano wa kuidhamini klabu ya Simba ukiwa na thamani ya Bilion 4.9 .
Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya michezo ya bahati
nasibu nchini Kenya imeweza kuingia nchini Tanzania na kuja kufanya
uwekezaji kwa klabu mbalimbali za mpira wa miguu.
Utiaji saini wa makubaliano ya mkataba huo umefanyika jioni hii
katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na wadau mbalimbali wa
mpira nchini.
Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva amesema mkataba huu utaweza
kuwasaidia katika kuendelea kutoa hamasa kwa timu yao kufanya vizuri
zaidi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa SportPesa nchini Abbas Tarimba amesema
kuwa wamefurahi sana kuingia mkataba na Timu ya Simba na mkataba wao
utakuwa katika hatua tofauti kulingana na makubaliano waliyoyaingia.
Amesema kwa mwaka wa kwanza Klabu ya Simba watapata milioni 880 na
katika miaka mitatu inayofuata watapata nyongeza ya asilimia 6 huku
mwaka wa mwisho wa mkataba huo klabu hiyo itafaidika kwa kupata bilioni
1.08.
Mbali na hilo Tarimba amesema kuwa klabu ya Simba itafaidika kwa
kupata fedha mbalimbali kama hamasa iwapo wataweza kupata ubingwa kwa
kupewa bonus ya milioni 100 au kushiriki michuano ya kimataifa.
Kabla ya utiaji saini wa mkataba huo
Simba iliweza kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya stand United magoli
yakifungwa na Laudit Mavugo na Juma Luizio huku la Stand likifungwa na
Kasim Selembe.