DAVIDO AKUBALI YAISHE....ARIDHIA MAOMBI YA SHABIKI WAKE
Davido amesema yupo tayari kuhudhuria siku hiyo ya kuzaliwa kwa shabiki yake huyo ili kuweza kuokoa maisha yake baada ya kuona malalamiko ya shabiki wake huyo aliyesema tangu 2014, alijaribu kutuma ujumbe, lakini hakufanikiwa kujibiwa wala kukutana naye.
“Wiki chache zilizopita kulikuwa na video ya shabiki wangu akitangaza kujiua kutokana na kunitafuta kwa muda mrefu bila mafanikio ya kuniona, hivyo sipo tayari kusababisha kifo chake, nitahakikisha nahudhuria siku hiyo ya kuzaliwa kwake ili niokoe maisha yake,” aliandika Davido kwenye ukurasa wake wa Instagram.


