BALOZI SEIF ALLY IDD AONGOZA DUA MAALUM YA KULIOMBEA AMANI TAIFA.
Waumini
wa Dini ya Kiislamu wakisoma Dua maalum ya kuliombea Taifa Amani na
Utulivu pamoja na kujiandaa kuukaribishwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
iliyofanyika katika Msiki wa Ijumaa Malindi Mjini Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar akijumuika pamoja na Waumini mbali mbali wa
dini ya Kiislamu Nchini katika Dua maalum ya kuliombea Taifa Amani na
Utulivu pamoja na kujiandaa kuukaribishwa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani. Kulia ya Balozi Seif ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh
Omar Ka’abi pamoja na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikha Alhad
Mussa Salum.
Mufti
Mkuu wa Tanzania Bara Sheikh Abubakar Zubeir Ali wa kwanza kutoka
Kushoto, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji pamoja na Mkuu wa
Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud walikuwa miongoni wa
Viongozi walioshiriki Dua
Baadhi
ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Madhehebu ya Shia Kutoka Nchini Iran
waliojumuipa pamoja na Waumini wa Zanzibar katika Dua ya kuliombea Taifa
Aman.
Maulamaa
na wahadhiri kutoka Nchini Misri nao walikuwa miongoni mwa washiriki wa
Dua hiyo iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Malindi.
Baadhi
ya Maimamu wa Misikiti mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi wakisoma
Dua hiyo maalum ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu pamoja na kujiandaa
kuukaribishwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa nasaha ya
kuwataka waumini na Wananchi kuendelea kudumisha Amani kwenye Dua ya
Kuliombea Taifa amani. Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Mkusanyiko wa
Waumini wa Dini ya Kiislamu katika mfumo wa kushikamana bila ya
kufarakana daima huzaa baraka zinazootesha neema na kheir miongoni mwa
Umma huo mtukufu mbele ya Muumba wao Mwenyezi Mungu.
Alisema
Vitabu vya Dini na Miongozo yote iliyotolewa katika Vitabu hivyo
imekuwa ikielekeza na kusisitiza umuhimu wa Binaadamu hasa Wale
walioamini Vitabu hivyo kushikamana pamoja ili lile lengo lao la
kumuabudu Mwenyezi Muungu likamilike bila ya kutetereka kwa kitu
chochote kile.
Balozi
Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa Dua Maalum ya kuliombea Taifa
Amani na Utulivu pamoja na kujiandaa kuukaribishwa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani unaokaribia kuingia wiki chache zijazo dua iliyofanyika katika
Msikiti wa Ijumaa Malindi Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Mamia ya
Waumini wa Dini ya Kiislamu, Wananchi pamoja na baadhi ya Viongozi wa
Serikali na Kisiasa.
Alisema
Waumini na Wananchi wote wanapaswa kuzingatia umuhimu wa suala la Amani
iliyopo Nchini kwani kwa kufanya hivyo kutatoa fursa kwa Waumini hao
kutekeleza kwa utulivu Ibada zao sambamba na Wananchi kuendelea na
harakati zao za Kimaisha za kila siku.
Aliwahimiza
Waumini wa Dini zote hapa Nchini kuendeleza Dua mbali mbali ambazo ndio
ufunguo wa Ibada yoyote ile inayomuelekeza Mja kudumu katika ucha Mungu
unaotakiwa kudumishwa katika mazingira yanayomzunguuka ya kila siku.
Balozi
Seif aliwashukuru Wananchi wa Kisiwa cha Pemba kwa mshikamano wao
waliouonyesha ndani ya kiindi hichi cha Mvua za Masika zilizoleta maafa
na kusababisha Mamia ya Wakaazi wake kukosa sehemu za Kuishi baada ya
nyumba zao kujaa maji na nyengine kuanguka kabisa.
Alisema
kitendo hicho cha mshikamano kimerejesha mafungamano ya Wananchi hao
kilichokosekana kwa kipindi kirefu kutokana na itikadi zao tofauti za
Kisiasa zilizosababisha kutengana na kuleta athari kubwa hata kwenye
maeneo ya Ibada katika kumcha Mwenyezi Mungu.
Akizungumzia
ujio la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuingia wiki chache
zijazo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitoa wito kwa
Wafanyabiashara wote hapa Nchini kuacha tabia ya kupandisha bei za
bidhaa muhimu zinazotumiwa kwa wingi na waumini wa Dini ya Kiislamu
katika kipindi hicho cha saumu.
Alisema
tabia hiyo mbaya ni dhambi kubwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
haitakuwa na huruma katika kuwachukulia hatua za kisheria
wafanyabiashara wowote watakaopandisha bei bidhaa zao bila ya sababu za
msingi zitakazokubalika.
Balozi
Seif alisema ni vyema kwa Wafanyabiashara kuwaonea huruma Waumini
watakaofunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao wengi kati yao wanaeleweka
upatikanaji wa kiato chao unakuwa na mazingira ya mashaka.
Mapema
Mufti Mkuu wa Tanzania Bara Sheikh Abubakar Zubeir Ali alisema Dua ni
fursa kubwa inayompa fursa Mwanaadamu kumuomba Mungu amuelekeze katika
njia ya Amani.Sheikh Zubeir alisema Mwenyezi Muungu muda wote hutarajia
kuombwa na waumini wake vyenginevyo anaondosha baraka zake na
kutowajaalia kheir na hatma njema waombaji hao anayoisisitiza kila siku
kufanywa na waja wake.
Hata
hivyo Mufti Mkuu huyo wa Tanzania alitahadharisha wazi kwamba zipo
ishara zinazoanza kujichomoza za mmong’onyoko wa Maadili unaotishia
kutetereka kwa Amani jambo ambalo kila Muumini na Mwananchi anapaswa
kuliondoa au kulikemea lisije kuleta athari hapo baadae.
Akimkaribisha
Mgeni rasmi katika Dua hiyo Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa
Ayoub Mohamed Mahmoud aliipongeza Kamati ya Amani ya Kitaifa Zanzibar
kwa juhudi inazochukuwa za kuhakikisha kwamba Taifa la Tanzania
linaendelea kuwa na utulivu.
Mh.
Ayoub alisema Dua hiyo ni tukio muhimu kwa Mustakabala wa Taifa hili na
aliwaomba Waumini na Wananchi wote popote pale walipo kuendelea
kuwaombea dua Viongozi wao waliojitolea kusimamia mapambano dhidi ya
Dawa za kulevya na Mmong’onyoko wa Maadili unaooneka kuliathiri Taifa
hasa kundi kubwa la Vijana.
Katika
shughuli hiyo ya dua Maalum ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu pamoja
na kujiandaa kuukaribishwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Masheikh na
Maulamaa wa Mkoa Mjini Magharibi wametoa zawadi Maalum kwa Rais wa
Zanzibar Al – Hajj Dr. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi
Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud.
Zawadi
hizo wamezitoa kutokana na mchango mkubwa wa Viongozi hao katika
kusimamia suala la Amani, mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya Nchini
pamoja na kuzuia mmong’onyoko wa Madili ulioonekana kupotea siku za
nyuma.
Dua
hiyo ya Ighaathatul – Mustaghiith ambayo pia husomwa kila jumatano
baada ya sala ya Ishaa katika Msikiti huo wa Ijumaa wa Malindi
iliongozwa na na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Kitaifa Zanzibar
Sheikh Salim Mohamed Hassan.


