Breaking News

WIKI MOJA BAADA YA AJALI YA WANAFUNZI WA LUCKY VICENT ARUSHA....HIKI NDICHO KINACHOENDELEA SHULENI HAPO.



Wakati wanafunzi  watatu majeruhi katika ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent  wakienda kwa matibabu nchini Marekani wanafunzi waliobaki shuleni leo wataendelea na masomo huku kukiwa na ukimya shuleni hapo.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Ephraim Jackson alisema jana kuwa shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa leo baada ya kufungwa kwa wiki moja.

Amesema ratiba masomo pia itapangwa leo ikiwepo siku za kuanza mitihani ya muhula.

Hata hivyo tofauti na siku nyingine jana  katika shule hiyo kilikuwa kimya hakukuwa na mwanafunzi.

Baadhi ya wafanyakazi eneo la usafi wa madarasa na magari walikuwa wakiendelea na usafi.