ZITTO KABWE AMTAKA AMTAKA MWIGULU NCHEMBA KUMCHUKULIA HATUA KALI ASKARI POLISI ALIYEMTISHIA BUNDUKI ADAMU MALIMA.

Zitto
kabwe ameonyesha masikitiko hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii
Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa kuwafanyia hivyo raia
wasiokuwa na hatia kiasi cha kuibua hofu katika jamii inayowazunguka na
kupoteza imani na jeshi hilo la polisi.
“Hii
ni nini ?, askari wetu wanafundishwa kufanya hivi, Waziri Mwigulu huyu
yupo wazi na ni wa kutoka kwako. Unahitaji uchunguzi”. Ameandika Zitto.
Zitto
aliandika hayo baada ya muda mchache kupita kwa tukio hilo
lililowahusisha askari hao walioambatana na kampuni ya Majembe Auction
Mart waliokuwa wakitaka kujaribu kukamata gari iliyokuwa imeegeshwa
pembeni ya barabara ya Masaki karibu na Hoteli ya Double tree ingawa
ndani ya gari hilo alikuwepo dereva.


