Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa ametangaza rasmi
kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta.
Kenyatta aliyeunga ushirika pamoja na
William Rutto, anaingia katika kinyang’anyiro cha kuwania awamu ya pili
ya kuiongoza Kenya huku upande wa upinzani ukiwa umepitisha jina la
Raila Odinga kupeperusha bendera ya upinzani.
Wakati Lowassa akitangaza kumuunga mkono
Kenyatta, kwa upande wake Odinga tayari ilishajulikana wazi urafiki wake
na Rais Dk. John Magufuli ambao umeanza miaka mingi tangu akiwa Waziri
wa Ujenzi.
Hatua hiyo ya Lowassa ambaye anatajwa
kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi nchini na Afrika Mashariki imekuja
baada ya kutembelewa jana nyumbani kwake Monduli na wabunge zaidi ya 20
na maofisa kutoka Kaunti ya Kajiado nchini Kenya.
Alisema ushawishi wake kwa Kenyatta
umejengwa na imani kubwa aliyonayo kwa Rais huyo akiamini kwa dhati
kwamba ana uwezo mkubwa wa kuwaunganisha wananchi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki na hasa Tanzania na Kenya.
Katika tamko lake, Lowassa mwanasiasa
mwenye ushawishi nchini Kenya pia kupitia jamii ya Kimaasai aliwasihi
wananchi wa Kenya kutokufanya makosa katika uchaguzi ujao.
Lowassa Ajiunga na Kenyatta Katika Safari ya Ushindi Nchini Kenya
Reviewed by Unknown
on
10:18 PM
Rating: 5