Mkali wa muziki wa hip
hop nchini Marekani, Shawn Carter ‘Jay-Z’ na mke wake, Beyonce,
wameonyesha namna wanavyoandaa maisha bora ya watoto wao mapacha
wanaowatarajia hivi karibuni.
Wakali hao wa muziki
duniani wametumia dola milioni 120, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 264 za
Kitanzania kununua nyumba kwa ajili ya watoto hao mapacha wawili.
Wapenzi hao, ambao ndoa
yao ina mvuto mkubwa na mfano wa kuigwa na mastaa wengi duniani,
wametumia kiasi hicho cha fedha kuwanunulia nyumba yao ili watoto hao
wakizaliwa waikute.
Eneo la nyumba hiyo
lina ukubwa wa eka mbili na linalindwa na ulinzi mkali kwa ajili ya
usalama wa mali zilizopo ndani ya eneo hilo.
Inasemekana kuwa, madirisha ya nyumba hiyo yamefungwa vifaa maalumu kwa ajili ya kuzuia kushambuliwa na risasi.
Nyumba hiyo ina jumla
ya vyumba 11 vya kulala, pamoja na sehemu ya kupaki magari 15, chumba
cha kutayarishia muziki na sehemu nne za wazi za kuogea (swimming pool).
Jay-Z na Beyonce Wanunua Nyumba ya Bilioni 264 Kwa ajili ya Watoto wao Mapacha
Reviewed by Unknown
on
10:13 PM
Rating: 5