Barnaba amedai kuwa ni bora fedha zao za muziki ziibiwe na
Diamond kupitia tovuti yake ya kuuza muziki ya Wasafi.com kuliko watu
wengine.
Muimbaji huyo ameiambia Dizzim Online, “Tumeibiwa sana wasanii,
tumedhulumiwa sana. Mungu anisamehe kidogo, bora atuibie msanii
mwenzetu, tunajua msanii mwenzetu anakula yupo kwenye soko letu kuliko
atuibie mtu binafsi.”
“Na yeye akiwa kama CEO [Diamond] alichukua uamuzi wa busara kama
heshima kutupigia simu wasanii wenzake mwenyewe kuliko kuwatuma
menejimenti. Mimi naona jambo zuri la bahati alilolifanya na nilienda
nikachukuwa contract yangu na kiukweli nimeusaini lakini bado
kuurudisha,” ameongeza.
Katika hatua nyingine hitmaker huyo wa ‘Lover Boy’ amewataja wasanii
ambao watasikika kwenye albamu yake mpya. Wasanii hao ni pamoja na
Baraka The Prince, Linex, Dela, H_art The Band, Bahati wa Kenya, Vanessa
Mdee kuna Jux, Maua Sama, G Nako na wengine.
Barnaba: Bora Atuibie Diamond Kuliko Kuibiwa na Mtu Binafsi.
Reviewed by Mipiko
on
9:08 AM
Rating: 5