Pamoja na baadhi ya wadau na mashabiki wa sanaa nchini
kuendelea kumtupia maneno machafu msanii wa muziki wa kizazi kipya
Harmorapa, msanii huyo anaonekana kuendelea kung’ara.
Producer na mtangazaji mkongwe wa redio na mmiliki wa Tetemesha
Production, Sandu Mpaka aka Kidboy, amesema licha ya changamoto ambazo
anakutana nazo msanii huyo za kutukanwa na baadhi ya wadau mbalimbali,
hali hiyo ndiyo inayosababisha vyanzo tofauti kumzungumzia na watu
kumuelewa zaidi.
Akizungumza na mtangazaji Manoni MJ wa Pili wa CG FM ya Tabora, Kid
amedai kuwa Watanzania wanahitaji burudani za aina tofauti hivyo watu
hawatakiwi kuhoji juu ya suala la Harmorapa kupewa airtime kwenye vyanzo
vya habari.
Kidboy Afunguka Kuhusu Harmorapa....Adai Mafanikio yake Yanatokana na Matusi Yanayomshambulia.
Reviewed by Mipiko
on
10:36 AM
Rating: 5