COSATO CHUMI: NITAHAKIKISHA SHULE ZOTE ZA MAFINGA MJINI ZINAKUWA KATIKA UBORA UNAOTAKIWA.

MBUNGE
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi madawti kwa viongozi
wa kata ya sao hill kwa ajili ya matumizi ya shule.


MBUNGE
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipongezwa na viongozi wa kata
ya sao hill kwa jitihada wanazozifanya kuleta maendeleo katika jimbo la
mafinga mjini.

Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo ya shule hii.
MBUNGE
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ameendelea kutatua changamoto
mbalimbali za jimbo hilo kwa kufanya ziara kwenye baadhi ya shule za
msingi zilizopo katika mjini wa mafinga na kukagua baadhi ya miundombinu
inayoendelea kukarabatiwa kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa
wananchi wake.
Katika
ziara hiyo Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo
wawili ya shule, mifuko 10 ya saruji, madawati 150 kwa shule za msingi
za Ifingo na Kinyanambo ambayo yalitolewa na wakala wa shamba la miti
Sao Hill huku chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mafinga Mji kupitia
mwenyekiti wake Yohanes Cosmas wakichangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili
ya kuunga mkono jitihada za mbunge za kukamilisha ujenzi wa miundombinu
hiyo.
Katika hatua nyingine mbunge huyo alitembelea jengo jipya la ukumbi wa
kisasa lililojengwa na kikundi cha Agape group ambalo lipo kwenye kata
ya Kinyanambo kwa lengo la kuinua kipato cha halmashauri hiyo.
Baada ya mbunge kuona jitihada hizo alichangia 300,000 huku chama cha
mapinduzi (CCM) wilaya kikichangia 100,000 kwa ajili ya kumalizia ujenzi
huo.
Shule ya Msingi Ifungo iliyopo wilayani Mafinga inakabiliwa na
changamoto ya miundombinu ikiwamo Umeme, maji ya bomba, madawati na
nyumba za walimu jambo ambalo limedaiwa kuwa kukosekana kwa umeme
kumesababisha wanafunzi kushindwa kufaulu vizuri.
Kilio hicho kimetolewa mwishoni mwa wiki na mwalimu mkuu wa shule hiyo
Tedy Captein wakati akizungumza mbele ya mbunge wa jimbo hilo Cosato
Chumi (CCM) wakati mbunge huyo akiwa kwenye ziara ya kutembelea miradi
ya maendeleo ya jimbo hilo.
Mwalimu Captein alisema baada ya rais John Magufuli kutoa elimu bure
wanafunzi wameongezeka na hivyo wanahitaji maji safi ya bomba badala ya
kuelendela kutumia maji ya tanki ambayo sio rafiki sana kwa wanafunzi
hao.
Hata
hivyo kutokana na ongezeko la wanafunzi wananchi wameamua kutumia nguvu
kazi yao kwa kujenga jengo la darasa moja pamoja na ofisi ya mwalimu
kwa gharama ya sh.Mil. sita hadi kufikia kwenye lenta lakini walishindwa
kumalizia.
Akijibu
kilio cha shule hiyo kuhusu umeme mbunge Chumi alianza kwa kusema
“Tutazungumza na shirika la umeme tanesco ili waweze kutuletea umeme
ambao utasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa shule hii.”alisema
Chumi.


