Mkali wa ‘Aje’ Alikiba amekwea pipa kuelekea nchini Marekani kwa ziara yake ya kimuziki katika miji tofauti nchini humo.
Alikiba aliwasili juzi kutokea nchini
Afrika Kusini alipokwenda kwa ajili ya ziara ya kimuziki pamoja na
kukabidhiwa tuzo yake aliyoshinda ya MTV EMA baada ya kuwashinda Wizkid
na Black Coffee.
Mdogo wa mwanamuziki huyo Abdulkiba
amesema kuwa Alikiba alikuja nchini kwa ajili ya kuleta tuzo hiyo na
kuondoka nchini kuelekea Marekani.
Abdulkiba amesema kuwa ratiba ya
mwanamuziki huyo kwasasa ipo tiati sana katika kufanya maonyesho ya
kimataifa na wakirejea watafanya kazi hapa nchini pamoja na nje ya nchi.
Alikiba Aelekea Marekani kwa ziara ya kimuziki
Reviewed by Mipiko
on
10:09 AM
Rating: 5