Hatimaye Mama Mzazi wa Diamond Atua Rasmi Bongo Muvi,Hii hapa Muvi Yake ya Kwanza.
Mama mzazi wa staa wa Afro-Pop, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’, ametua rasmi kwenye
fani ya uigizaji wa sinema za Kibongo (Bongo Muvi).
Akizungumza na gazeti hili katika
mahojiano maalum, mama Diamond alitamba kwenda kimataifa kwenye upande
wa filamu kama anavyofanya mwanaye Diamond akiwa ameshiriki katika
utayarishaji na uigizaji wa filamu iitwayo Mtepela iliyochezewa huko
Kibirizi mkoani Kigoma.
“Nimefanya hiyo filamu na wasanii wa Kigoma, nawajua vizuri lakini kwa sasa siwezi kuizungumzia zaidi,” alisema mama Diamond.
Kwa upande wa mtayarishaji
aliyeshirikiana naye aliyejitambulisha kwa jina la Isaya Lazaro
almaarufu Zito, alisema mama Diamond mbali na kushiriki katika
utayarishaji wa filamu hiyo pia alitoa fedha na ni mmoja wa waigizaji
waliofanya vizuri ndani yake.
“Tulimwandalia scene (vipande),
akavicheza lakini kabla ya kumaliza alipata safari ya kwenda Afrika
Kusini na baada ya kurejea tuendelea kuimalizia”, alisema Zito


