Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amefanya ziara
ya kushtukiza katika kiwanda cha kuzalisha Konyagi, Tanzania
Distilleries kilichopo Chang’ombe na kukuta bado kinazalisha pombe aina
ya viroba.
Makamba aliongozana na
timu ya watu kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA), Jeshi la Polisi na Baraza la Mazingira (NEMC).
Katika ukaguzi huo
walikuta shehena yenye katoni zaidi ya 100,000 ya viroba vya konyagi na
valuers vilivyoonyesha kuendelea kuzalishwa hadi jana ikiwa ni siku ya
mwisho ya tangazo la katazo la kuzalisha pombe hiyo.
Pia wamebaini sehemu ya
mitambo zilipokutwa pombe hizo zilionyesha mtambo huo umezimwa ghafla
huku pombe ikimwagika sakafuni, hata hivyo uongozi wa kiwanda hicho
walikuwa wanalazimisha kuwasha CCTV ili kuwaonyesha mitambo hiyo
ilizimwa lini.
Meneja wa kiwanda hicho
Davis Deogratius, amegoma kusaini fomu ya idadi ya mzigo aliokutwa nao
hadi alipolazimishwa na hatimaye kukubali ambapo, alilalamikia hatua
hiyo huku akieleza hasara watakayoipata kutokana na kutouza mzigo huo.
Januari Makamba Akamata wazalishaji wa Viroba Chang'ombe
Reviewed by Mipiko
on
9:05 AM
Rating: 5