TAZAMA PICHA:MZEE WA MIAKA 78 ANAYESOMA DARASA LA KWANZA TARIME

Mzee Nyamhanga Suguta (78) mkazi wa kijiji cha Getenga kata ya Mbogi
wilaya ya Tarime mkoani Mara akiwa ndani ya darasa la kwanza katika
shule ya msingi Makerero baada ya kuamua kuanza kusoma darasa la kwanza

Mzee akiwa paredi na wanafunzi wenzake

Muda wa kwenda nyumbani mzee akiwa paredi
******
Mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la Nyamhanga Suguta Gesaba (78) mkazi
wa kitongoji cha Kibeyo Kijiji cha Getenga kata ya Mbogi Wilayani Tarime
Mkoani Mara ameamua kujiunga na masomo ya shule ya msingi na kuanza
darasa la kwanza katika shule ya msingi Makerero.
Mzee huyo anasema lengo kuanza kusoma ni kujua kusoma ,kuandika na
kuhesabu ili kuendeleza biashara zake ndogo ndogo za kuuza ndizi.
Mzee Huyo amesema kuwa hakubahatika kwenda shule kipindi cha ujana wake
hivyo alianza mwaka jana kwenda shule na akabahatika kufaulu na hivyo
ameamua kujiunga darasa la kwanza ili kutimiza ndoto yake kwani elimu
haina mwisho.
Walimu wa mwanafunzi huyo wanasema maendeleo yake shuleni ni mazuri.


