Tunda Man ni msanii wa bongofleva ambaye makazi yake ni Dar es salaam
ambapo February 3 2017 Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda
alizungumza kwenye makao ya Polisi kituo cha kati na kusema miongoni mwa
watu atakaowahitaji wakamuone Jumatatu kwa ishu ya dawa za kulevya ni
pamoja na Tunda.
Kwa sababu mkuu wa mkoa hakutumia majina halisi ya kuzaliwa, watu
mbalimbali walianza kumpigia simu msanii Tunda Man baada ya kuambiwa
jina lililotajwa na Makonda ni Tunda.
Baada ya simu za kutosha Tunda Man aliamua kuandika Instagram kwamba sio
yeye aliyetajwa bali aliyetajwa ndio huyo kwenye picha, akaambatanisha
na picha ya Mrembo Tunda ambaye ameonekana kama video queen kwenye video
za bongofleva.
Tundaman aliandika
‘Jamani Tunda aliyetajwa na Muheshimiwa @PaulMakonda ni huyu na sio
mie maana simu zimekua nyingi, @Sudibrown na wewe hujui au umeamua
kunipigia tu…
Msanii Tundaman Afunguka Haya Baada ya ‘Tunda’ Kutajwa Kwenye List ya Makonda
Reviewed by Mipiko
on
7:06 PM
Rating: 5