Kiongozi wa
upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi,
amefariki dunia mjini Brussels nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka
84.
Tshisekedi alikwenda mjini Brussels mwishoni mwa mwezi jana kwa ajili ya matibabu.
Bwana Tshisekedi alikuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe waliokuwa mstari wa mbele kupigania demokrasia ya nchi yake.
Alisimama kidete katika utawala wa aliyekuwa
kiongozi wa nchi hiyo Rais Mobutu Sese Seko, ambae utawala wake ulidumu
kwa miongo kadhaa kabla ya kupinduliwa.
Etienne Tshisekedi pia
alikuwa mpinzani wa Rais Laurent Kabila, ambae aliingia madarakani mnamo
mwaka 1997, na mwanae, Rais Joseph Kabila, ambae hivi sasa ndio
anatawala nchi hiyo.
Kiongozi wa upinzani DRC Etienne Tshisekedi afariki dunia
Reviewed by Mipiko
on
7:39 PM
Rating: 5