Msanii wa Bongofleva Darassa ambaye kwa sasa anafanya vizuri na hit
single ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Muziki’ ameamua kuweka wazi mtazamo
wake kuhusu ile video iliyosambaa ikionesha vijana wakicheza wimbo wake
huku dereva akiacha gari likienda.
Vijana hao wamekamatwa na polisi na Darassa ameamua kutoa mawazo yake
kuhusiana na kitendo hicho ambacho kimewafanya vijana hao kukamatwa na
polisi Itigi Singida, Darassa ametuamia account yake ya instagram
kuandika ujumbe kuoneshwa kuguswa na kitendo hicho...
“Hawa ndugu zetu nimepata taarifa wamekamatwa kwa kosa la kutaka
kusababisha ajali na unaweza kuona Kama mchezo ulielekea kubaya,
ingeweza kua Tatizo kwao Au kumu sababishia mwingine, Naskia watakua
mahakamani Leo I’m not so sure naendelea kufatilia”
“Nawaombea Tatizo hili Mungu awafanyie wepesi I’m sure wamejifunza
Hawawezi kufanya tena mistake Kama Hii itokee, mizuka feelings mtu
anaweza kufanya kitu njee ya mipango yake sometimes, Mungu awasaidie
🙏🏽 LENGO NI KUJENGA DUNIA KUA SEHEMU NZURI NA SALAMA KUISHI #Muziki“
Soma Aloichokiandika Darassa Baada ya Dereva Kukamatwa Akicheza Wimbo Wake Huku Akiendesha Gari
Reviewed by Mipiko
on
7:43 PM
Rating: 5