Breaking News

Morogoro;Kijana atiwa mbaroni kwa kujifanya askari POLISI








Kamanda wa Polisi mkoa wa MOROGORO, URLICH MATEI

Jeshi la polisi mkoani MOROGORO linamshikilia mtu mmoja SHABANI MZIBA mkazi wa mji mpya manispaa ya MOROGORO kwa kosa la kujifanya Afisa wa Jeshi hilo mwenye cheo cha ASP.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro ULRCHI MATEI amesema mnamo Novemba 30 mwaka huu, majira ya saa 11 jioni maeneo ya KINGOLWIRA manispaa ya MOROGORO mtuhumiwa alijifanya  yeye ni afisa wa jeshi hilo na kughushi  mhuri wa kituo cha polisi kati MOROGORO kinyume cha sheria.

 Mtuhumiwa SHABANI MZIBA anadaiwa kuwa alighushi muhuri wa kituo cha polisi cha kati morogoro na kumwandikia barua MAZAO NGALE mkazi wa Mkono wa Mara akimtaka waonane kujadili kesi inayomkabili ya kuoa mtoto mdogo.

Katika tukio lingine jeshi la polisi mkoani Morogoro limemfikisha mahakamani mtu mmoja  aliyefahamika kwa jina la KAJUNA RWEYEMAMU mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam na kisha kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa lawizi wa shilingi milioni 3.