Wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wanaoishi Hosteli ya Mabibo
wamekusanyika usiku wa jana kwenye lango la kuingilia, huku wakiimba
wakiwataka viongozi wa Serikali ya Wanafunzi UDSM (Daruso) kuja
kusikiliza kilio chao.
Huku
wakiimba nyimbo mbalimbali ikiwamo ‘Kama siyo juhudi zako Nyerere…nchi
hii ingekuwa wapi’ na ule maarufu wa ‘Solidarity forever’, walidumu
kwenye mkusanyiko huo takriban kwa saa mbili hadi saa 6.15 waliopoamua
kuondoa baada ya viongozi wao kutofika.
Wakizungumza
kwa sharti la kutotajwa, baadhi ya wanafunzi walisema wanaishi maisha
ya shida kutokana na kutolipwa fedha za kujikimu na kwamba, mateso hayo
yamesababishwa UDSM, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Serikali na Bodi
ya Mikopo.
Hatua
hiyo ilisababisha magari mawili ya polisi yaliyosheheni askari kupiga
kambi eneo hilo, lakini kiongozi wao alisema hiyo ni doria ya kawaida
ikiwa ni sehemu ya majukumu yao.