MREMBO GIGY MONEY ATOA YA MOYONI....ATAJA MAMBO YANAYOMUWEKA MJINI

Video
queen ambaye haishiwi vituko, Gigy Money amefunguka kwa kusema kuwa
mauno yake ya mwendokasi ndio kitu ambacho kinawafanya wasanii wengi
wamtafute kwa ajili ya kufanya naye kazi.
Mrembo huyo ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM, amesema kuwa video queen ni kazi ambayo inalipa tofauti na watu wanavyofikiria.
“Unajua
kazi yoyote ukiiheshimu ni rahisi nayo ikakuheshimu,” alisema Gigy
Money. “Mimi hii kazi naiheshimu ndio maana imeniweka mpaka hapa nilipo.
Sasa hivi mimi ni mtangazaji wa kituo kikubwa cha redio, kwa hiyo mimi
naweza kuwaambia watu wanatakiwa kuiheshimu hii kazi kama kazi
nyingine,”
Aliongeza,”Kusema
kweli sasa hivi mimi ni moja kati ya video queen ambao tunafanya kazi
nyingi lakini haya yote yanatokana na nikipata kazi naifanya isavyo,
napiga mauno ya mwendokasi mpaka mtu labda alipanga kunipa scene moja
anajikuta nanipa mbili au tatu,”


