Breaking News

ZIARA YA RAIS WA ZAMBIA YALETA NEEMA NCHINI....TANZANIA NA ZAMBIA ZAKUBALIANA KUIMARISHA RELI YA TAZARA


Serikali za Tanzania na Zambia zimeahidi  kuimarisha  utendaji kazi wa reli ya TAZARA  na mradi  wa bomba la mafuta la TAZAMA yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa  baina ya nchi hizo.mawaziri-tz-na-zambia

Akizungumza  leo,  Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais wa Zambia Edgar Lungu  amesema kuwa Tanzania na Zambia zitaendelea  kushirikiana kuiboresha  reli hiyo ili iweze kufanya kazi  kwa ufanisi.rais-edgar-lungu-zambia

Kwa upande wake Rais John Pombe Magufuli amesema Reli  ya TAZARA na bomba la Mafuta la TAZAMA zinakabiliwa na changamoto za mtaji na uongozi na hivyo kufanya reli hiyo kuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo tani 128,000 tu, ambapo ilipoanzishwa mwaka 1976 ilikua na uwezo wa kubeba mizigo tani 500,000.

Ili kutatua changamoto hizo Rais Magufuli amesema kuwa “tumekubaliana kubadilisha  menejimenti ya TAZARA, kubadilisha sheria ili kuwezesha menejimenti hiyo kuongozwa na  mtu mwenye uwezo  ambaye si lazima awe anatoka Tanzania au Zambia”.rais-jpm

“Nia ya Serikali hizi ni kuongoza reli hiyo kibiashara  kwa maslahi na maendeleo ya nchi zote mbili” alisema Rais Magufuli.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli malengo ya Serikali zote mbili ni kupunguza ucheleweshaji mizigo  kufika nchini Zambia, ambapo wamekusudia  kupunguza vituo vya kukagua magari ya mizigo hadi kufikia vinne.tanzania-na-zambia

Sambamba  na hayo Serikali hizi mbili zimesaini makubaliano ya kuwepo kwa mashaurinao ya kidiplomasia, pamoja na kuahidi kuendeleza ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili.