Kupendwa raha! hivyo ndivyo unaweza kusema baada ya staa kwenye tasnia
ya mitindo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kumuandikia mpenzi wake, Ali Kiba
‘King Kiba’ ujumbe mzuri ambao amedai umetoka kwenye sakafu ya moyo
wake.
Mwanamitindo huyo ambaye yupo karibu zaidi na mkali huyo wa wimbo ‘Aje’,
kupitia ukurasa wake wa instagram, jana alimsifia msanii huyo huku
akiichambua show yake aliyoifanya usiku wa kuamkia Jumapili katika
tamasha la Fiesta Dar es salaam.
Maneno ya Jokate haya hapa:

Komando Kipensi @officialalikiba kwanza thank you for trusting me and @noelgiotz
to style you for Fiesta- tulielewa how important this day is to you and
I’m glad we made it . It was fun creating this iconic look, you made it
easy though I mean your body is just perfect and the way you carry
yourself with so much class and honor you just gave this outfit the life
and sophistication it needed. Style yako ya mavazi ni ya kipekee,
hugezi mtu unatengeneza yako kama unavyofanya na mziki wako, ni halisi.
Sasa mimi napenda kuongea nikiguswa, sio kama AK ila baada ya kuona
ulichofanya jana kwenye stage ya fiesta ( umeimba live na band kwenye
umati mkubwa vile kwa ustadi mkubwa kabisa mpaka watu wakashtuka maana
you were simply perfect ) naomba kusema tu wewe hushindani na yoyote
hapa Tanzania, kuanzia ladha yako ya mziki unaotengeneza mpaka sauti
yako – tena huko kwenye sauti naomba nisiongee maana sitaki upasuke
bichwa lako lol ila kuna kitu cha kipekee kwenye sauti yako, you are
“The Voice”. Kila siku unakuwa bora zaidi yaani labda nikufananishe na
Beyonce kimziki- usiniue lakini . Ukitaka you can dance, you can sing
tena live sauti cleeeear haina mikwaruzo, you can rap, unaeeza igiza
uchizi yaani you are just perfect kama mwanamuziki. Kama hujui leo ujue.
Nakuombea siku mmoja dunia nzima iweze kufurahia hiki kipaji adhimu
kutoka kwako. Unajua kuna tofauti ya kuimba wimbo au kusikiliza wimbo tu
kama burudani na kusikiliza kitu kinachokuinua spiritually. Kitu
kinagusa roho yako. Nikisikia Aje, Mwana, My Everything, Mali yangu hata
kama nina mood mbaya vipi my soul becomes happy yaani naturally. You
are a gem na utafika tu. Huu mwendo wako huu huu ndio poa.
Wasikuchanganye. Nikiangalia mfano wa Wizkid yeye anafanya mziki wake,
focus yake niyeye na fans wake na ndio maana yuko alipo licha ya
kushindanishwa na watu kutwa nzima. Blood fans wa AK najua mko nae
tumlazimishe huyu kijana afanye tour nchi nzima pekee yake labda . Haya
mambo ni makubwa wallahy. All in all I’m very proud of you na your
journey of growth and WTH man start giving me credit on the lyrics I
help you with . Hongera @cloudsfmtz kwa show nzuri na kwa wasanii wote #Kajiandae