Mbowe amesema kikao hicho kilifanyika mnamo tarehe 25/10/2016 saa
mbili usiku na kiliongozwa na Waziri Mkuu akiwa na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahaman Kinana.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe katika kipindi
cha Maswali kwa Waziri Mkuu leo amedai kuwa, mnamo siku ya Jumanne
tarehe 25/10/2016 saa mbili usiku kiliitishwa kikao cha wabunge wa CCM
ambacho Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa Mwenyekiti, na kilihudhuriwa
na Katibu MKuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwa ajili ya kujadili
Muswada wa Habari.
Mbowe amesema kuwa Wabunge wakiwemo Mawaziri walihongwa shilingi
milioni 10 kila mmoja ili waweze kusaidia kupitisha Muswada wa Habari
unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni kesho.
Lakini Naibu spika amekataa katakata Waziri mkuu kujibu swali la
Mbowe kwa waziri mkuu kuhusu tuhuma hizo za wabunge wa CCM kuitwa kwenye
kikao na kupewa fedha kiasi cha milioni 10 kila mmoja ili wasiibane
serikali kwenye muswada wa sheria unaowasilishwa kesho
Maelezo ya Naibu spika ni kuwa swali hilo halihusu sera, huku Mbowe akidai linahusu sera kwa kuwa ni rushwa kwa wabunge
Freeman Mbowe Aja na hii Mpya...Adai Wabunge wa CCM wamehongwa kitu Kidogo ili kupitisha Muswada wa Habari
Reviewed by Mipiko
on
8:27 AM
Rating: 5