Raia wa Tanzania
aliyeshtakiwa kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi la chuo kikuu cha
Garissa 2015 ambapo takriban watu 149 waliuawa amepata ugonjwa wa
kiakili akiwa jela.
Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini
Kenya, Rashid Charles Mberesero aligunduliwa kuwa hawezi kuendelea na
kesi baada ya ripoti ya daktari wa maswala ya kiakili kusema kuwa
amekuwa akitibiwa tatizo la kuwa na ''tabia mbaya'' katika jela ya
kamiti.
Gazeti hilo linasema kuwa ameshtakiwa pamoja na Mohamed Ali Abdikar,Hassan Aden Hassan,Sahel Diriye na Osman Abdi.
Wamekana mashtaka 162 ya ugaidi.
Kulingana
na Daily Nation,siku ya Jumatano,upande wa mashtaka ulitaka kupewa muda
kujadiliana jinsi ya kuendelea na kesi hiyo dhidi ya wenzake kutoka
Kenya.
Matokeo ya ripoti ya ukaguzi wa akili iliowasilishwa katika
mahakama ilisema kuwa alidungwa sindano yake ya kila mwezi mnamo tarehe
12 mwezi Septemba.
''Amekuwa akikabiliwa na matatizo yasio ya
kawaida ,ambapo anaamini watu wote karibu naye wana nia za
kishetani'',daktari Mucheru Wang'ombe aliandika katika ripoti hiyo.
Kulingana na Daily Nation,daktari huyo amesema kuwa mshukiwa huyo anahitaji matibabu na uchunguzi wa kila mara wa akili yake.
''Ripoti
hiyo inasema kuwa mshukiwa huyo apewe matibabu katika hospitali ya
Mathare kila mwezi na hayuko katika hali yake kuendelea na kesi hiyo na
kwamba majadiliano yanaendelea'',alisema kiongozi wa mashtaka Eddie
Kadebe.
Mtanzania apata tatizo la kiakili akiwa jela Nchini Kenya
Reviewed by Mipiko
on
11:24 PM
Rating: 5