Mahakama
Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi imefuta kesi iliyofunguliwa na Mbowe
Hotels Ltd. dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa Shirika hilo
liliitoa kampuni hiyo katika jengo lake jijini Dar es salaam kwa
kufuata taratibu zote na kuzishikilia mali zake kihalali.
Uamuzi
huo umetolewa asubuhi hii na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema
madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba
mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.
Mlalamikaji
alikuwa wakidai kwamba wakati NHC inamtoa kwenye nyumba alikuwa ndani
ya Mkataba wa Ubia na NHC, lakini Jaji alikataa hilo na kusema ingawa
Mkataba wa Ubia Ulikuwepo lakini kwa kuwa haukutekelezwa ipasavyo. Na
wakati wa NHC kumtoa kwenye nyumba Walikuwa na Mahusiano ya Mwenye
Nyumba na Mpangaji, Mahusiano ambayo yako wazi kisheria juu ya
Utekelezaji wake.
Mawakili
wa Mbowe Hotels Mhe. John Mallya na Mhe. Peter Kibatala (pichani )
wakiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu
kutoka, wakidai kwamba hawakuridhika na uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa
kesi ya mteja wao.