Wapatanishi katika
mazungumzo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema kuwa pande
husika zimekubali kuhusu mpangilio wa uchaguzi utakavyofanyika,swala
ambalo lilifanya upinzani kujiondoa katika meza ya mazungumzo mapema
wiki hii.
Tuhuma kwamba huenda rais Joseph kabila akajaribu
kujiongezea muda wa kutawala baada ya muhula wake wa pili kukamilika
imesababisha mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Waziri wa haki Alexis
Thambwe Mwamba amesema kuwa chini ya makubaliano hayo ambayo hayajatiwa
saini,uchaguzi wa urais,ule wa kitaifa pamoja na ule wa kijimbo
itafanyika siku moja.
Bwana Mwamba ameongezea kwa serikali ya mda
ikishirikisha wanachama wa upinzani itabuniwa ili kusaidia kutatua
mgogoro huo wa uchaguzi.
Makundi mengi ya upinzani yamesusia mazungumzo hayo ili kutohalalisha mchakato wa mazungumzo hayo.
Mapema
shirika la Amnesty International lilichapisha ripoti ambayo ilishtumu
mamlaka ya DRC kwa kupanga njama za kuwakandamiza wapinzani wa Kabila.
Upatanishi wa Kisiasa wazaa Matunda nchini DRC.
Reviewed by Mipiko
on
8:25 PM
Rating: 5