
China imepeleka madaktari
watano mkoani Kagera, Tanzania, kusaidia kutoa matibabu kwa watu
walioathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea jumamosi iliyopita na
kusababisha vifo vya watu 17 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa China nchini Tanzania imesema,
madaktari hao ni pamoja na madaktari wa magonjwa ya wanawake, watoto,
upasuaji, na wa magonjwa ya kawaida.
Ujumbe wa mabalozi kutoka nchi mbalimbali nchini Tanzania pamoja
na jamii ya wafanyabiashara ulitoa mchango wa dola za kimarekani laki 7
na vifaa vingine vya kuwasaidia watu waliokumbwa na maafa hayo.