Breaking News

Mwanamke mrembo alizwa na penzi la Harmorapa ‘nimetoka Mwanza kuja kufunga naye ndoa, nitamlipia kila kitu’

Wahenga wanasema mapenzi ni upofu hakuna anayeweza kuzuia hisia pale anapokuwa amempenda mtu na hili limekuja kudhihirika kwa mrembo Khadija ambaye ametoka Mwanza hadi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuwinda penzi la Harmorapa.


Khadija na Harmorapa
Khadija akizungumza kwenye kipindi cha eNews cha EATV amesema kuwa ametoka Mwanza kuja kufunga ndoa na Harmorapa kwani walishawahi kutana naye Mwanza na waliahidiana kuoana.
Nimekuja kutoka Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya harusi na baby wangu Harmorapa, mara ya kwanza kabisa Harmorapa alikuja kwenye show Mwanza. Kwa sasa ni miezi miwili tangu nikutane naye na namlea,“amesema Khadija.
Kwa upande mwingine Khadija amesema yupo tayari kugharamia gharama zote za ndoa kwani anampenda sana Harmorapa.
Hata hivyo, Harmorapa mwenyewe amekanusha taarifa hizo na kudai kuwa mwanamke huyo hamfahamu na anamharabia jina lake.