Upelelezi unaonesha askari hawakushiriki kwenye mauaji ya Akwilina hivyo wameachiwa – Mambosasa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa ameweka wazi kwamba askari waliokuwa wanashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha Usafirisaji, NIT, Akwilina Akwilina walikwishaachiliwa kutokana na upelelezi kuonesha hawakuhusika.
Kauli hiyo ya Mambosasa imekuja leo wakati alipokuwa akijibu swali la nini kinachoendelea dhidi ya askari ambao waliwekwa rumande wakati wa upelelezi uliokuwa ukihusisha mauaji ya mwanafunzi huyo ambaye alipigwa risasi Februari 16 mwaka huu.
Kamanda Mambosasa amesema kwamba “ni kweli askari walishikiliwa ili kufanyika uchunguzi katika mauaji yale, na mazingira ya kifo yalielezwa vizuri. Upelelezi ulionesha Askari hawakushiriki kwenye mauaji hayo ila kilichosababisha ni maandamano haramu ambayo yalisababisha watu kukusanyika vurugu zikatokea milipuko ya risasi ambayo ilipelekea tukio lile kutokea. Wale askari walitoka kutokana na jalada lilipopelekwa kwa mwanasheria ilionekana kuna udhaifu ndiyo maana hawajashtakiwa“.
Mbali na hayo, Kamanda Mambosasa ameongeza kwamba pamoja na kuwa inahisiwa askari ndiyo waliorusha risasi kwenda kwa waandamanaji, hisia hizo haziwezi kutengeneza kosa.
“Hisia hata ziwe nzito kiasi gani hazitengenezi kosa ninachosema ni matokeo ya upelelezi. Kesi iliyopo ni waandamanaji waliosababisha tukio kutokea. Viongozi waliokuwepo kwenye maandamano wote wana silaha ingawa hatujajua ni silaha ya nani ilitumika” ameongeza.
Akwilina aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT aliuawa kwa kupigwa risasi wakati Jeshi la Polisi likiwatawanywa waandamanaji wa CHADEMA, Kinondoni Jijini Dar waliokuwa wakielekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho.
Hata hivyo kwa sasa viongozi wa juu wa CHADEMA pamoja na wabunge saba wa chama hicho kwa sasa wanakabiliwa na kesi Na. 112/2018 katika mahakama ya Kisutu ambapo moja ya mashtaka yanayowakabili ni kufanya maandamano haramu yaliyopelekea mauaji ya mwanafunzi Akwilina.