Breaking News

WIZARA YA AFYA NCHINI KENYA YAAGIZA WAPISHI HOTELINI KUFANYIWA UCHUNGUZI


Waziri wa afya nchini Kenya Cleopa Mailu ameagiza wapishi wote wanaohudumia katika Hoteli na Migahawa kufanyiwa uchunguzi wa matibabu kufuatia mliipuko wa kipindupindu kaunti ya Nairobi. 

Mailu amesema hatua hii ina lengo la kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo ambao tayari umesababisha vifo vya watu watatu. Akizungumza katika kaunti ya Kitui, Mailu pia amesema wachuuzi wa vyakula na maji hawataruhusiwa kuendeleza biashara zao.