Breaking News

TAZAMA VIDEO: NEYMAR APIGANA AKIWA MAZOEZINI BARCELONA....UBUYU WOTE UPO HAPA

Hali ya mambo ndani ya Klabu ya Barcelona inaonekana haipo sawa baada ya mchezaji wa timu hiyo Neymar kukwaruzana na kushikana na mchezaji mwezake wa timu hiyo.
 
Neymar amevurugana na beki mpya kikosini hapo Nelson Semedo wakati walipokuwa katika mazoezi ya jana Ijumaa asubuhi.
Baada ya tukio hilo, Neymar aliondoka mazoezini hapo wakati program ikiwa bado haijamalizika. 
Neymar amekuwa akihusishwa kutua PSG kwa dau la pauni milioni 191, yawezekana tukio hilo likaongeza presha kubwa katika tetesi hizo za uhamisho wake.