BABU WA KITAA MZEE WA "TEGUA MTEGO" AFUNGA NDOA ILIYORUSHWA LIVE INSTAGRAM
Mtangazaji na mfanyakazi wa Clouds Media Group (CMG) Kaiza Sosa maarufu kama Mapanki jana Jumapili amefunga ndoa na mke wake huku akionekana mwenye furaha zaidi.
Mapanki ambaye ni mwendeshaji wa kipindi cha "Tegua Mtego" kinachorushwa kupitia Clouds Tv amefunga ndoa ya kufana ambayo ilirushwa live kupitia akaunti yake ya Instagram.






