KIKWETE AMTEMBELEA MWADHAMA KARDINALI PENGO DUBAI

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amemtembelea Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, nchini Dubai leo.
Kikwete
ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter leo(Ijumaa) na
kueleza kuwa amemkuta Kardinali Pengo akiwa mwenye siha njema.
Ingawa
hajaeleza amemkuta Kardinali Pengo nyumbani au Hospitali lakini askofu
huyo mkuu wa jimbo la Dar es Salaam, amewahi kuripotiwa kuwa yupo nje ya
nchi kwa matibabu.
“Nikiwa
Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama
Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema.”
Ameandika Kikwete
Kikwete amesema amemtembelea Kardinali Pengo wakati akiwa safarini kuelekea Canada.

Nikiwa Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema. pic.twitter.com/aWNIwOuToN— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) June 16, 2017


