ZARI AMJULIA HALI MZAZI MWENZAKE IVAN SSEMWANGA HOSPITALINI.

Ivan ambaye alipata watoto watatu na Zari, anadaiwa kukimbizwa hospital wiki hii baada ya kupoteza fahamu.
Jumatatu hii Zari alipost picha ya mshumaha na kuwaomba mashabiki wake kumuombea mzazi mwenzake huyo.
Hapo jana Zari kupitia ukurasa wake wa SnapChat aliandika “Siku mbili kwangu zimekuwa ngumu, nawaomba tumuombee Ivan”.
Mitandao ya Uganda inadai kuwa Ivan anasumbuliwa na maradhi ya Shambulio la Moyo (Coronary Artery Disease).


