MRISHO MPOTO ATUKANWA NA MASHABIKI.....MWENYEWE AFUNGUKA NA KUTAJA SABABU ZA KUTUKANWA KWAKE.

Mrisho Mpoto ameeleza kwa nini ameamua kumuunga mkono Rais Magufuli na amesema ataendelea kumuunga mkono.
“Nimepokea
matusi mengi, kebehi, na maneno machafu juu ya mimi kuunga mkono
utendaji wa Rais Magufuli, kitu ambacho nakiamini kuna “KUKUBALIANA KWA
KUTOKUBALIANA” lakini siyo kumtukana mtu mwingie siyo busara hata kidogo
“Kwakuwa
tu hakusema au hakufanya ambacho nafsi yako ilipenda kusikia.
Kilichonifanya niandike ujumbe huu ni kuwa nisiwekewe maneno mdomoni
yakuwa nimesema Rais Magufuli ni Mungu, kwa wale ambao hawakuangalia
sherehe za MEI MOSI jana
“Naomba
niseme kuwa hayo maneno siyo kweli na yamebadilishwa kutoka kwenye
ukweli wa niliosema, Mimi ni mtu mwenye hofu na Mungu siwezi kusema
hivyo, kumekuwa na utamaduni ikitokea mtu anauunga mkono utendaji wa
Rais kuna ibukuka kundi la wapinga Maendeleo na kuanza kutukana
“Naomba
ijulikane kuwa sababu za kumuunga mkono Rais, yale niliyokuwa nayaongea
huko nyuma naona yanafanyiwa kazi hivi sasa!! MRISHO MPOTO mpaka sasa
namuunga mkono Rais MAGUFULI, Iwe nachumia tumbo kama inavyosemwa au
nimevimbilwa kwa shibe.


