Breaking News

Klabu ya Yanga Yakiri Kudaiwa Mil.300


Klabu ya Yanga imethibitisha kudaiwa kodi takribani shilingi Milioni 300 na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambayo ni kodi ya jengo la Kaunda liliopo eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa klabu ya klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameweka bayana jambo hilo baada ya kuenea kwa taarifa zinazodai kuwa jengo hilo lipo hatarini kupigwa mnada kutokana na deni la Shilingi 300.

huku akisema tangu mwaka 1996 na 1997 Klabu haijawahi kulipa kodi hiyo japokuwa kipindi hicho ilikuwa ni rahisi lakini wamejipanga kulipa  kutokana kesi yao kuwepo Mahakamani

"Ni muda mrefu kodi hii ilikuwa haijalipwa tangu mwaka 1996 na 1997 Klabu hajaiwahi kulipa kodi hiyo japokuwa ilikuwa ni rahisi lakini miaka ya karibuni imekuwa ikiongezeka na ninavyosema tunatakiwa kulipa Milioni 56 na laki 6 kwa mwaka...Sisi kama viongozi tunafanya jitihada kubwa za kuweza kuinusuru jengo letu na Mungu akijalia itawezekana". Alisema Mkwasa

Kwa upande mwingine, timu ya Yanga inatarajiwa kushuka dimbani kesho kuvaana na Tanzania Prisons katika michuano ya Shirikisho la Tanzania Bara unatakaopigwa katika viunga vya uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.