Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kuongeza kima cha chini cha
mshahara kwa asilimia 18, ili kuwapunguzia watu wenye mapato ya chini
athari zinazotokana na mfumuko wa bei uliofikia asilimia 11.5 katika
miezi 57 iliyopita.
Kwenye sherehe ya siku ya wafanyakazi iliyofanyika Nairobi, rais
Kenyatta amesema ongezeko hilo linalenga kupunguza matatizo
yanayowakabili watu wa tabaka la chini nchini humo.
Rais Kenyatta pia ametoa amri ya kuongeza bonasi isiyotozwa kodi
na malipo ya muda wa ziada hadi kufikia dola elfu 1 za kimarekani, ili
kuwasaidia watu wenye mapato ya chini.
Kenya Yaongeza Mshahara wa Kima cha Chini kwa asilimia 18
Reviewed by Unknown
on
8:07 AM
Rating: 5