Hussein
Machozi amesema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa
Radio na kudai kuwa yeye alikwenda Kenya kikazi na mtu ambaye alikuwa
anawasiliana naye alikuwa ni binti aliyeandaa show yake Kenya, hivyo
alipofika alimpokea Airport na kwenda naye hotel.
"Kwa hiyo tulipofika hotel
tulikuwa tunapanga mipango ya hapa na pale, kumbe yule binti ana
mshikaji wake ambaye ana wivu sana na yeye, hivyo yule jamaa alikuja na
magari kama mawili yakiwa na mabaunsa kibao, wakatuzunguka pale na
kuanza kunipiga vibao ila nashukuru Mungu kuna baunsa mmoja pale pale
alinishtua na kuniambia nikimbie, hivyo niliruka ukuta wa hotel na
kukimbia. Kwa hiyo wale wahudumu pale ndiyo walianza kusambaza habari
kuwa nimefumaniwa ila nisingekimbia huenda ingekuwa mbaya kwangu" alisisitiza Hussein Machozi
Mbali na hilo Hussein Machozi anasema
alimua kwenda nchini Italia baada ya kuona muziki unampa mawazo hivyo
Mungu akamfungulia mlango mwingine na kuamua kusepa huko, ambako anadai
anasoma na kufanya shughuli zingine zinazomuingizia kipato.