Nchi ya Urusi imechukizwa na uamuzi wa Marekani wa kuishambulia kambi ya jeshi la anga mjini Homs nchini Syria kwa makombora.
Maafisa wa Marekani walisema kuwa
waliilipua kambi hiyo kwani ndiyo iliyotumika kuendeleza shambulizi
liliotumia silaha za kemikali yenye sumu katika mji unaodhibitiwa na
waasi, ambapo watu kadhaa walipoteza maisha siku ya Jumanne.
Lakini Urusi inaunga mkono serikali ya Rais Bashar al-Assad na imekashifu shambulizi hilo ambalo linadaiwa kuua watu sita.
Shambulio hilo linajiri siku chache tu
baada ya shambulio la gesi ya sumu lililolengwa katika mji wa Khan
Sheikhoun, mkoa wa Idlib liloua zaidi ya watu 80, wengi wao wakiwa
watoto.
Upinzani wa Syria unasema kuwa ni serikali ya Syria iliyotekeleza shambulio hilo lakini serikali ya Assad inapinga haya.
Inadaiwa kuwa sasa Urusi inaweza kufanya uamuzi wa kuboresha mtindo wa Syria wa kulipua makombora.
Kwa muda mrefu Syria ilikuwa na mfumo
ulio fana sana wa ulinzi wa anga zake lakini vita ambavyo vimekuwa
vikiendelea umeudhoofisha.
Urusi nayo ina mfumo wa kisasa zaidi wa
kurusha makombora kutoka ardhini hadi hewani katika kambi yake ya Syria
lakini kwa sababu zisizoeleweka hawajaweza kuzuia mashambulizi ya
Waisraeli.
Urusi Yachukizwa na Marekani Kuishambulia Syria.
Reviewed by Unknown
on
12:24 PM
Rating: 5