DIAMOND PLATINUMZ AFUNGUKA SABABU YA KUACHIA SONG LA "ACHA NIKAE KIMYA"
Baada ya Diamond Platnumz kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Acha Nikae Kimya’ mwanamuziki huyo ameamua kuelezea sababu ya kutoa wimbo huo kipindi hiki.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Diamond ameelezea sababu ya kuachia wimbo unaoelezea amani ya nchi.
Diamond aliandika kama ifuatavyo
Ili Nchi ipate maendeleo inahitaji
Upendo na Ushirikiano wa Wananchi na Serikali..Na Nikiwa kama Msanii,
jukumu langu ni kuhakikisha natumia Hekma na busara kukemea jambo
nilionalo haliko sawa ili lirekebishwe, lakini pia panapokuwa hakuna
maelewano jukumu langu pia ni kupatanisha ili kwa pamoja tujenge nchi
yetu kusudi wazazi wetu, watoto pamoja na familia zetu waishi kwa Upendo
Amani na kufurahia nchi yetu…Na ndiomaana kwenye nyimbo nakwambia “MI
NA WEWE WA TAIFA MOJA…KAMBARAGE BABA MMOJA….SASA TOFAUTI ZA NINI
TUSHIKAMANE TUKAIJENGE TANZANIA”… Unatakiwa utambue kuwa kila kiongozi
ni Binadamu na kama wote tujuavyo, Binadamu hatujakamilika… hivyo katika
nchi yoyote lazma wakati mwingine kuna jambo linaweza likawa haliko
sawa, ila sisi kama wananchi tunatakiwa tutumie Hekima na Busara kwenye
kufikisha ujumbe ama hoja zetu ili viongozi walieke sawa…Busara na
Hekima itafanya viongozi watuelewe kirahisi na pengine mengi tuyatakayo
tutimiziwe kirahisi… mfano mzuri, juzijuzi kupitia kipindi cha Clouds360
cha clouds Tv nlipopata bahati ya kuongea na Mh Raisi nilimuomba
atufungulie Mabanda ya Chipsi na Bodaboda ziruhusiwe kufanyakazi hadi
asubuhi maana zilikuwa nwisho saa 4 ama 5 usiku…kwakuwa nilitumia Hekima
na busara kwenye Kufikisha hoja ama Ombi langu..alikubali na tukapewa
ruksa na sasa hivi maeneo mengi ya Chipsi na Bodaboda yanafanya kazi
hadi usiku mnene… hivyo tusikubali tu kulishwa Sumu za kuleta ugomvi
kati yetu wenyewe kwa wenyewe eti Mara Tutukane mara sijui fanyeni hiki,
wakati hata baadhi ya wanaochochea mambo hayo hawaishi Tanzania
wanaishi Ulaya / Marekani / kifupi nje ya nchi…ikija kutokea bahati
mbaya kimenuka wao watakuwa wanakula kuku kwa mrija huko walipo…halafu
sisi na familia zetu ndio tutateseka na kuhaha kunusuru roho zetu usiku
kucha.. Hatutaki makelele ya Uchonganishi mitandaoni, kama mtu kweli
anauchungu na nchi na kweli akisemacho anamaanisha aje, na kwa pamoja
twende sehemu husika kupeleka malalamiko sio kukaa kitandani kupost
kuchochea Ugomvi kumbe anatuchora na kutufanya kama sie mataahira wake,
anatupeleka mara kushoto mara kulia… Akikaa pekeake anatucheka kuwa sie
wajinga wake katueka mkononi…


