KUTOKA CUF:WATU SITA WAKAMATWA NA POLISI KWA KUTAKA KUSABABISHA VURUGU
Mtu mmoja akiwa na wenzake wapatao 5 ambao wanasemekana kua wafuasi wa chama cha Chadema wamekamatwa wakiwa kwenye ofisi za Chama Cha Wananchi CUF wakifanya usafi huku ikisemekana kua hiyo ilikua njama ya kuleta vurugu katika eneo hilo.
Akihojiwa na jeshi la polisi mmoja wa watuhumiwa ambae inasemekana kua ndie mlengwa mkuu amedai kwamba amekuja tu kufanya usafi lakini baada ya kubanwa sana akafunguka kuwa ametumwa na watu wa chama kingine(CHADEMA) ili wakafanye vurugu hapo ofisini
Tuhuma hizi zinakuja wakati kukiwa na migogoro baina ya vyama hivi







