Kesi inayomkabili Salum Njwete
(Scorpion) ya kumtoboa macho Said Ally imeendelea jana katika mahakama
ya wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Wakati wa kesi hiyo Deus Johakim Magosa
(45) ambaye ni shahidi wa nane upande wa Jamhuri katika kesi hiyo
alinusurika kutupwa lupango baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali,
Nassoro Katuga kumtuhumu kutoa ushahidi wa uongo.
Wakili Katuga alimtuhumu shahidi huyo
kutokana na kutoa majibu tofauti wakati akimuongoza kutoa ushahidi wake
na maelezo aliyoyatoa awali Kituo cha Polisi cha Buguruni.
Awali shahidi huyo alisema mahakamani
hapo kuwa hakuwahi kusikia popote kuwa Scorpion amehusishwa katika tukio
la kumshambulia Said, lakini baadaye alipobanwa alisema ni kweli
alisikia tetesi hizo kuwa mtuhumiwa huyo ndiye aliyefanya tukio hilo.
Pamoja na mambo mengine aliyomhoji na
kumbaini kuwa anatoa ushahidi wa uongo wakili Katuga alipomgeukia hakimu
aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Flora Haule na kumwambia shahidi
anazidi kuidanganya mahakama hiyo na kuitaka mahakama hiyo imchukulie
hatua kwa mujibu wa kifungu cha 164 cha ushahidi hapa nchini (Tanzania
Evidence Act).
Shahidi huyo alionekana kuwa katika
wakati mgumu baada ya wakili huyo kuwaita askari polisi na kuwataka
wakae tayari kumchukua shahidi huyo.
Kutokana na ufinyu wa muda hakimu Flora
aliahirisha kesi hiyo mpaka Aprili 18 mwaka huu na kumuacha shahidi huyo
aondoke na kumtaka kufika tena mahakamani hapo tarehe iliyopangwa bila
kukosa ambapo Scorpion naye alirudishwa mahabusu mpaka tarehe hiyo.
SHAHIDI KATIKA KESI YA "SCORPION" APONEA CHUPUCHUPU KUWEKWA LUPANGO....KISA KIPO HAPA
Reviewed by Unknown
on
8:38 AM
Rating: 5